Kuhusu   Dira   Dhamira  Huduma zinazotolewa  Mawasiliano

 

Mkulima library ni kitengo kinachotoa huduma ya habari na taarifa kwa wakulima hapa nchini Tanzania na hata nje ya nchi, ambacho kimeanzishwa na Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Umuhimu wa kilimo nchini Tanzania ni mkubwa kwa kuwa unabeba uti wa mgongo wa uchumi wa nchi hii tangu enzi za zamani hata leo, na kwa ajili hii kitengo hiki cha aina yake kinawaangalia wakulima kama sehemu muhimu katika uchumi wa taifa. Kwa hiyo kitengo kimejikita katika kutoa kwa mapana huduma ya habari na taarifa za kilimo kwa wakulima mmoja mmoja na sekta binafsi kwa kutumia mtandao wa teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Nia ni kutoa taarifa kulingana na mahitaji ya wakulima nchini kote ikiwa ni pamoja na maeneo ya vijijini ambako huduma nyingi za taarifa na habari hazifiki wa urahisi. Huduma hii itawezesha wakulima kupata taarifa muhimu za ugani na nyinginezo kufuata matakwa ya wahitaji wa taarifa hizo ili zitumike katika kuinua kilimo na uchumi wa mtu binafsi hata wa taifa zima kwa ujumla. Wakulima wanaweza kupata taarifa hizi kwa ama kutembelea tovuti ya kitengo...., au kwa kufika moja kwa moja katika Maktaba ya SUA ambapo watakutana na huduma ya kiuweledi itakayokidhi mahitaji yao ya taarifa husika.

Pamoja na watumiaji/wahitaji wa taarifa kujihudumia wenyewe kwa njia ya mtandao, pia kitengo kinatoa mafunzo ya mtu mmoja mmoja au vikundi kwa muda mfupi ya namna ya kutumia njia za kisasa za TEHAMA kupata taarifa na habari mbalimbali, kutoa rufaa au huduma ya maelekezo ya mahali pa kupata msaada wa zaidi kufuatana na uhitaji wa taarifa ulivyo.

Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine inapenda kuchukua fursa hii kutangaza kuanzishwa kwa “Mkulima Library” pamoja na kuwakaribisha wote kuitumia katika kujipatia habari, taarifa na maarifa ya Kilimo chenye tija.

Dira

Mkulima Library inalenga kuwa kituo chenye sifa za kipekee cha kuwahudumia wakulima wa aina mbalimbali kwa mahitaji ya taarifa na habari za kilimo katika mapana yake hapa nchini Tanzania

Dhamira
 
Kwa kutumia teknolojia za kisasa zilizo rafiki kwa watumiaji wote na wahudumu wenye uweledi, kitengo kitawahudumia wakulima wa aina mbalimbali kwa mahitaji yao ya taarifa na habari pamoja na kusambaza taarifa hizo katika namna ambayo itawafikia wakulima wengi ndani na nje ya nchi.


Huduma zinazotolewa

  • Machapicho ya aina mbalimbali (print na electronic)
  • Video za programu za wakulima
  • Muda mfupi kwa ajili ya mafunzo ya matumizi ya Tehama kwa wakulima na maofisa ugani wanaotembelea kitengo hiki
  • Maswali na majibu kwa njia ya mtandao
  • Sehemu tulivu ya kujisomea
  • Kutoa nakala za machapisho (photocopy)
  • Scanning

Mawasiliano (Contact)

Kwa mawasiliano zaidi, tafadhali unaweza
Kutuma barua pepe (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.)
Kupiga simu. 0754415464, 0754317440
Kutuma ujumbe mfupi wa maneno. 0754415464, 0712309086

 
Machapisho

Yako kwenye matengenezo

Taarifa zaidi kupitia